VODACOM YAFUNGIA VOCHA ZA SH.500


Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom imezifungia baadhi ya vocha za sh.500, kutokufanya kazi baada ya kiripotiwa na mawakala kuwa zimeibiwa

Msemaji wa kampuni hiyo Matina Nkulu, aliyasema hayo baada ya wakazi wa eneo la Kibamba wilayani Ubungo  jijini Dar es salaam, kulalamika kuwa wamekuwa wakuuziwa vocha za 500 ambazo zimekuwa hazifanyi kazi

Nkulu amesema kuwa kampuni hiyo inataarifa za kuibiwa kwa vocha hizo tangu wiki iliyopita na wanaendelea na uchunguzi  juu ya tatizo hilo aidha Nkurlu amesema kuwa wamefikia hatua ya kufungia vocha hizo mara baada ya msambazaji wa kuripoti kuwa zimeibiwa

“Nimefuatailia hili tukio na inaulikana kuwa zimeibiwa nyingi tu kwa hiyo huyu msambazaji akaripoti Kwetu, hivyo ikabidi zote zifungiwe na ndiyo maana wateja wakinunua hazifanyi kazi” alisema Nkulu