Harmorapa amefunguka kuhusu kumiliki bastola yake binafsi

Rapper huyo machachari ambaye kila kukicha huteka vichwa vya habari kutokana na vituko vyake, amefunguka kuwa japo ana mali nyingi kwa sasa lakini hafikirii kuwa na bastola kwakuwa ana ulinzi wa kutosha.

#Harmorapa👉“Sasa hivi nina pesa nyingi, nina gari nini. Lakini sijawaza au kufikiri siku nije kumiliki bastola kwa sababu eti nina pesa sijawaza kwa muda huu ila sijajua huko mbeleni iatkuwaje,” amekiambia kipindi cha Dj Show cha Radio One,

Aliongeza👉“Nikisema kwaajili ya kujilinda unajua sasa hivi mimi nina bodyguard wangu ameshiba na ameenda hewani. Hata ninapokaa kwenyewe nina ulinzi mpaka umfikie Harmorapa kuna kazi kubwa sana na unaweza usionane naye," .