HAWA NDIO WASANII WA MAREKANI AMBAO WATAUZA NYIMBO ZAO KUPITIA WASAFI. COM

Mwaka jana tarehe 28 Disember, Diamond Platnumz pamoja na meneja wake Sallam sk walithibitisha kuwa kuna collabo ya Diamond pamoja na mega superstar wa Marekani Jay Z . . .
Akiongea na Clouds Fm hapo jana Diamond alisema kuwa wimbo huo upo tayari ila bado wapo katika maongezi na jay z katika maswala ya promotion, “wimbo wangu mpya na Jay Z upo tayari ila tunasubiri tu makubalino katika upande wa kuipromote ngoma kwenye soko la kule kwa sababu lengo la kufanya wimbo huu ni kwaajili ya kujulikana zaidi kwenye soko la marekani" alisema Diamond . . .
"wimbo huu pia ndio utafanya mtandao wangu wa wasafidotcom ukue maana wakati naenda kushoot video ya hii ngoma kuna baadhi ya wasanii kutoka marekani tuliweza kuzungumza kibiashara ili nyimbo zao tuziweke kwenye tovuti yetu ya wasafi.com" Diamond hakuweza kuweka wazi wasanii hao wa marekani ambao nyimbo zao zitapatikana #wasafidotcom ila alimtaja mmoja ambae ni Kanye West . .
Hata hivyo Diamond ameongeza kuwa kolabo hiyo ilizaliwa pale alipokutana na kanye west Las vegas Marekani kwani yeye ndie aliyemkutanisha na Boss huyo wa Roc Nation, na kuchukua miezi sita tu mpaka wimbo huo kukamika pamoja na kushoot video . .
DJ Khaled na ukubwa wake wote, alitumia mwaka mzima ili kumpata kwaajili ya kumshirikisha kwenye album yake ya mwaka jana, Major Key.

SIKU YA WAJINGA "HABARI HII SIO YA KWELI"