SERIKALI YA ZIMBABWE YAPITISHA SHERIA YA KUTUMIA MIFUGO KULIPA ADA ZA SHULE


Serikali ya Zimbabwe imeruhusu wazazi kulipa ada kwa mifugo au kwa kufanya kazi ktk shule husika kama malipo.

Waziri wa Elimu, Dr. Lazarus Dokora amesema kwamba mamlaka za shule zinatakiwa kubadilika na kuacha kufukuza watoto kwa kuwa tu wazazi wao hawana pesa.

Hii inakuja siku chache tu baada ya Waziri wa Fedha kupeleka Muswada bungeni wa kuamuru benki kukubali mifugo kama dhamana ya kuchukulia mikopo.

Zimbabwe inakabiliwa na uhaba wa pesa tangu mwaka jana baada ya Serikali kutishia kutaifisha makampuni yote ya kigeni nchini humo.

Benki zililazimika kupunguza kiwango cha kutoa pesa hadi $40 kwa siku kwa kila mtu mmoja.