TANZIA BABA YAKE BELLE9 AMEFARIKI DUNIA

Msanii Belle 9 amefiwa na baba yake mzazi mzee Damian aliyefariki usiku wa kuamkia leo akipatiwa matibabu baada ya kupata ajali. . . Meneja wake, Jahz Zamba, amesema kuwa Mzee Damian amefariki dunia baada ya kugongwa na boda boda iliyokuwa kwenye mwendo mkali huko mjini Morogoro alikokuwa anaishi.

Alivunja mguu mmoja pale pale na kujeruhiwa vibaya kabla ya kupelekwa hospitali. Dereva wa boda boda naye ameumia vibaya ikiwemo kuvunjika taya na kujeruhiwa kichwa. Jahz amesema baada ya Mzee Damian kupelekwa hospitali na kuwekwa kwenye wodi ya wagonjwa mahtuti, kuna dawa zilikuwa zikihitajika lakini zilikosekana kwenye hospitali hiyo. Amesema kaka yake Belle anayeishi Morogoro aliingia mtaani kuzisaka na aliporudi mida ya saa sita usiku alikuta Mzee ameshafariki.

1 comments:

When it comes to musical groups or bands doing live call-in radio interviews, it can be quite disastrous if there is no sense of order or direction. Without an 'interview plan' group members will talk all over each other and create frenzy for themselves and the radio host. Tanzania Music