ZLATAN AKATAA KULIPWA MSHAHARA MAN U


Imeripotiwa kuwa mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic amekataa kulipwa mshahara na klabu ya Man United kwa kipindi chote ambacho atakuwa akijiuguza goti lake.

Zlatan ,35,ameumia goti lake la kulia wiki iliyopita katika mechi ya Europa ligi dhidi ya Anderlecht na anataraji kufanyiwa upasuaji nchini Marekani na kukaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi 9, hivyo kurejea uwanjani ni mpaka mwakani 2018.

Kiasi ambacho angepokea kwa kipindi hicho ni Pauni Milioni 13, lakini raia huyo wa Sweden ameona si vizuri kupokea pesa hiyo wakati hachezi.

Zlatan ametua United majira ya kiangazi mwaka jana ambapo alisaini mkataba wa mwaka mmoja, akilipwa pauni 250,000 kwa wiki na pia kikiwepo kipengele cha kuongeza mkataba wa mwaka mmoja endapo pande zote zitafikia makubaliano.

Latest