CHADEMA kwa mara nyingine tena wamesitisha maandamano ya UKUTA



CHADEMA kwa mara nyingine tena wamesitisha maandamano ya UKUTA iliyokuwa imepangwa kufanyika Oktoba Mosi ili kupisha mbinu nyingine mbadala.

Wakati huohuo, CHADEMA imesema haimtambui Profesa Ibrahim Lipumba kama Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Taifa na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).