Hili Ndio Daraja litakalojengwa Dar Baada ya Daraja la Kigamboni

Ujenzi wa Daraja la Salender lenye urefu wa km 7 ikiwemo 1.4 baharini litakalounganisha ufukwe wa Coco na eneo la Aga Khan kuanza mwakani na kukamilika 2020.





















Hayo yamesemwa leo Ikulu na Rais Magufuli alipompokea mgeni wake Balozi wa Korea ya Kusini. Na hili litakuwa Daraja la pili kujengwa Baada ya Daraja la Kigamboni kukamilika ujenzi wake na kuanza kutumika na wakazi wa Dar es salaam hasa wa maeneo ya Kigamboni.