Taarifa ya (TFF) kuhusu kusitisha kwa muda kuutumia Uwanja wa Uhuru

Mechi mbili za raundi ya sita za Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Majimaji, na African Lyon na Kagera Sugar sasa zitachezwa kwenye Uwanja wa Taifa badala ya Uwanja wa Uhuru.

















Mabadiliko hayo yametokana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kusitisha kwa muda kuutumia Uwanja wa Uhuru katika kipindi hiki ambacho wameanza kufanyia marekebisho sehemu ya uwanja huo ambayo ni ya nyasi bandia (artificial turf). Hivyo, mechi ya Simba na Majimaji itafanyika Jumamosi, Septemba 24 wakati ile ya African Lyon na Kagera Sugar itachezwa Jumatatu, Septemba 26. Jumapili, Septemba 25 Uwanja Taifa utatumiwa kwa mechi ya timu za Wabunge za Simba na Yanga ili kuchangia waathirika wa janga la tetemeko lililotokea mkoani Kagera.