Walichosema Polisi kuhusu Mikutano ya ndani ya Vyama vya Siasa leo Agosti 22




















DAR: Polisi wamesema wameondoa rasmi zuio la mikutano ya ndani ya Vyama vya Siasa. Wadai wameridhika na hali ya kiusalama nchini.

Hata hivyo polisi imesisitiza kwamba maandamano na mikutano ya hadhara ya Vyama vya Siasa bado imezuiliwa isipokuwa kwa wabunge katika majimbo yao.

Hii inakuja baada ya Mwezi Septemba ambapo Polisi walizuia Mikutano yote ya ndani ya Vyama vya Siasa nchini.