Waziri Mkuu amewasimamisha kazi maofisa misitu

Waziri Mkuu amewasimamisha kazi maofisa misitu 4 na kusitisha uvunaji wa misitu eneo hilo kwa kutoridhishwa na usimamizi.

Maofisa waliosimamishwa kazi ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Dk. Paul Ligonja, Ofisa Misitu wilaya Gaudens Tarimo, Ofisa Misitu Yonas Nyambuya na Ofisa wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) wa wilaya Seleman Bulenga.