Wolper na Timu Wolper wamuunga mkono Paul Makonda na katika Project ya Mti Wangu Agosti 1

Maneno ya Wolper kuhusu kumuunga mkono Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda..

My people .. Kwanza niwashukuru kwa ushirikiano wenu siku zote, fans wangu nawapenda sana.. Hakuna jambo nalianzaga mnaacha kunisapoti.  Kwa kuanzia hapo Mimi kama Mkazi wa Jiji la Dar chini ya Mkuu wetu @paulmakonda nimeamua kwa moyo wangu kama mfano kwa jamii yangu kumuunga mkono katika project ya #MtiWangu ambayo inalenga kupanda miti na kutunza mazingira.
Naamini muda mwingine hata neno langu tu kwa nyie wapenzi linaweza kuleta shinikizo ,
Nawaomba mniunge mkono katika kumsapoti kaka yangu ninaependa kazi zake na jitihada zake katika kuimarisha jiji letu.
Swala la mazingira sio la serikali pekee, ni letu sote.. Na vizazi vijavyo.
Tuweke alama kwamba tuliishi kipindi hiki.  Chukua hata elfu Tano kanunua mche wa mti mmoja au zaidi na upande mahali.. Kila siku jioni chukua nusu saa umwagilie huku unajiamini unabadilisha kitu.. Huo mti utakuja kuokoa maisha ya wengi..
Tumezaliwa kusaidiana na kulindana
Tuungane na Mh. @paulmakonda kuokoa vizazi vijavyo, kutunza mazingira na KUPANDA MITI.