Alikiba akanusha kutumbuiza kwenye shindano la Miss Tanzania 2016



Alikiba amekanusha taarifa zilizoenea kuwa atatumbuiza kwenye shindano la Miss Tanzania 2016 litakalofanyika Jumamosi hii mjini Mwanza.

Taarifa hizo zilizosambaa zimedai kuwa Alikiba na Christian Bella ndio wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo lakini Kupitia mtandao wa Instagram, hitmaker huyo wa wimbo wa ‘Aje’ ameandika, “Taarifa Muhimu : Napenda Kuwajulisha Ya Kuwa Sitakuwepo.”
Tamasha hilo litakuwa likifanyika mkoani humo kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo nchini.