Uongozi wa Kagera Sugar umewasimamisha wachezaji wake wawili kwa tuhuma za kupokea rushwa



Uongozi wa Kagera Sugar umewasimamisha wachezaji wake wawili golikipa Hussein Sharif ‘Casillas’ na beki Erick Kyaruzi kwa tuhuma za kupokea rushwa ili kuihujumu timu wakati wa mchezo wa iliopoteza kwa kufungwa magoli 6-2.

Wamesimamishwa kwa muda usiojulikana ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili “Tunaendelea na uchunguzi kwa sababu kunaonekana kulikuwa na hujuma katika mechi yetu na Yanga kwa hiyo tumeona tuendelee na uchunguzi na tumeona wakae kando wakati tunaendelea na uchunguzi huo.” “Aina ya magoli tuliyofungwa kila mtu aliyaona na yanatia wasiwasi mkubwa. Suala sio idadi ya magoli suala ni aina ya magoli mtu aliyofungwa, hata kama ni goli moja lakini kama linatia wasiwasi lazima tuchukue hatua.” “Makosa ya namna ile hatukuridhika nayo ndiyo maana tunafanya uchunguzi. Hata beki goli alilofungisha unaona dhahiri kwamba halikupashwa kuwa goli ndiyo maana tunafanya uchunguzi.” alisema Katibu wa Klabu hiyo Hamisi Madak