Mahakama yawahukumu miaka 10 jela watu 2 waliohusika kutungua helikopta




SIMIYU: Mahakama yawahukumu miaka 10 jela watu 2 waliohusika kutungua helikopta ya kampuni ya Mwiba Holdings mwezi Januari, 2016.

Waliokumbwa na hukumu hiyo ni Doto Huja Kubeja na Mwigulu ambapo katika kesi hiyo walikuwa wanakabiliwa na mashitaka mawili ya kumiliki silaha na kumiliki risasai kinyume cha sheria. Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mrio amesema Mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri.