GEORGE LWANDAMINA: Historia ya Kocha Mpya wa Yanga



DONDOO MHIMU KUHUSU GEORGE LWANDAMINA.
- Jina lake kamili George Lwandamina.
- Tarehe ya kuzaliwa 5 August 1963 ( miaka 53 )
- Alikuwa anacheza nafasi ya ulinzi enzi za uchezaji.
- Kwa sasa ni kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Zambia.
- Pia ni kocha mkuu wa Zesco ya Zambia.
- Amekwisha fundisha vilabu vya Mufulira Wanderers, Green Buffaloes, Kabwe warriors, Red Arrows, Zesco United na timu za taifa Zambia za umri tofauti.
-Amepata elimu yake ya ukocha katika nchi za Ujerumani na Uholanzi.

ELIMU YA UKOCHA NA MAFANIKIO.

I.NGAZI YA VILABU
- Baada ya kuachana na kucheza soka, aliteuliwa  kuwa kocha msaidizi wa Mufulira Wanderers!akaiwezesha klabu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi kuu mara mbili mfululizo.(1995 , 1996)
- Baada ya kumaliza mafunzo ya ukocha nchini Ujerumani akateuliwa kuwa kocha mkuu wa Mufulira baada ya kocha mkuu kufariki January 1997.
- Akaiwezesha Mufulira kufika robo fainali ya klabu bingwa barani Afrika kisha akatwaa BP Challenge Cup.
-Mwaka 2000 akahamia Nchanga Rangers akiwa katika program ya kukuza vijana.
- Mwaka 2001 akajiunga na Green Buffaloes akiwa kocha Msaidizi.Mwaka huo huo akateuliwa kuwa kocha mkuu baada Kaumba kuondoka, aliifundisha klabu hiyo hadi mwaka 2008.
- akahamia Kabwe Warriors ambapo alikorofishana na viongozi wake baada ya kutumia muda mwingi kuihudumia timu ya taifa ambako alikuwa kocha msaidizi.
-akahamia Red Arrows ambako aliiwezesha kushika nafasi ya pili (2011), kombe la Barclays .
- Mwaka 2014 akahamia ZESCO mwaka huo huo akashinda ubingwa wa ligi kuu ya Zambia mara mbili mfululizo na kombe la Barclays.
-ameifikisha Zesco hatua ya nusu fainali klabu bingwa barani Afrika, ambapo ilitolewa na Mamelodi Sundowns kwa goli la ugenini ambao wakaja kuwa mabingwa (2015-2016)
-akachaguliwa kuwa kocha bora wa Zambia mara mbili mfululizo.

II. NGAZI TIMU YA TAIFA.
-Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Zambia U-20, kutoka mwaka 2003 hadi 2008, alibeba ubingwa wa COSAFA, akaiwezesha kufika nusu fainali ya michuano ya vijana Afrika, akaiwezesha kufuzu kombe la dunia kwa vijana nchini Canada wakaishia hatua ya 16 bora.
- Mwaka 2005 hadi 2006 alikuwa kocha msaidiizi wa Kalusha Bwalya katika timu ya Taifa ya Zambia.
-akawa kocha msaidizi wa Herve Renard kisha mwaka 2010 kocha wa muda baada ya Renard kujiuzulu.
-2015 akateuliwa rasmi kuwa kocha mkuu wa "The Chipolopolo", akaiwezesha kufuzu fainali za mataifa ya Afrika, ambapo Zambia waliongoza kundi lao lakini wakatolewa kwa penati na Guinea katika hatua ya robo fainali.