Taasisi ya SIKIKA inayojihusisha na masuala ya afya imeitaka Serikali kutoa majibuuhalisia ili kuonyesha ukubwa wa tatizo la uhaba wa dawa nchini



Taasisi ya SIKIKA inayojihusisha na masuala ya afya imeitaka Serikali kutoa majibu yenye ukweli, weledi na yanayoendana na uhalisia ili kuonyesha ukubwa wa tatizo la uhaba wa dawa nchini, badala ya kupiga siasa.
Tamko hilo limekuja siku 6 baada ya Wizara ya Afya kukanusha taarifa za nchi kukabiliwa na upungufu wa dawa unaoathiri afya za wananchi.