TRUMP: CLINTON ATAANZISHA VITA KUU VYA TATU VYA DUNIA SYRIA



Mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump amesema mpango wa mpinzani wake Hillary Clinton kuhusu kutatua mzozo Syria utaanzisha "Vita Vikuu vya Tatu vya Dunia". Amesema Marekani inafaa kuangazia zaidi kushinda vita dhidi ya kundi linalojiita Islamic State badala ya kulenga kumshawishi au kumshinikiza Rais wa Syria Bashar al-Assad kung'atuka uongozini.

Bi Clinton amekuwa akipendekeza kutolewe marufuku ya ndege kutopaa katika anga ya Syria, mpango ambao baadhi wanasema huenda ukasababisha mgogoro na ndege za kivita za Urusi ambazo zinatekeleza mashambulio dhidi ya waasi wanaompinga Bw Assad.

Maafisa wa kampeni wa Bi Clinton wamemtuhumu Bw Trump kwa "kuwachezea Wamarekani kupitia wasiwasi wao". Bw Trump pia amewashambulia wafuasi na viongozi wa Republican ambao wamekataa kumuunga mkono.

#BBC  -