ZLATAN KUJENGEWA SANAMU SWEDEN

Chama cha Soka cha Sweden (SvFF) kimetangaza kuwa watajenga sana ya Zlatan Ibrahimovic,kwenye mji wa Stockholm. Hii imekuja baada ya mshambuliaji huyo kushinda tuzo ya mwanasoka bora wa Sweden mwaka 2016, ambapo ni mara yake ya 10 mfululizo kushinda tuzo hiyo ambayo amechukua mara 11 kwa ujumla.



Sanamu ya mshambuliaji huyo ambayo itakuwa na urefu wa mita 2.7, itajengwa nje ya dimba la Friends Arena, katika mji mkuu wa Sweden.

Mshambualiaji huyo,35, wa Man United amecheza mechi 114 katika timu ya Taifa ya Sweden na kuifungia magoli 62 kabla ya kutundika daruga baada ya michuano ya Euro 2016