APIGWA NA GLASS USONI KWA KUONGEA KISWAHILI MAREKANI

Mwanamke mmoja raia wa Marekani mwenye asili ya Afrika amemsaheme mtu aliyempiga na bilauri (glass) ya kunywea bia usoni sababu alisikika akiongea kiswahili.



Asma Mohamed Jama aliyekuwa pamoja na familia yake wakipata chakula cha usiku katika mgahawa Oktoba 30, 2015 nchini Marekani alisikika akiongea lugha ya kiswahili ndipo Jodie Burchard-Risch (43) aliyekuwa jirani naye akampigi na bilauri na kisha kukimbia.

Kufuatia tukio hilo, Jama alipata majeraha sehemu mbalimbali za uso wake ikiwa ni pamoja na kwenye pua, sikio la kulia na mdomo wa chini. Alieleza kuwa baada ya tukio hilo kutokea limeyabadilisha maisha yake ambapo alikuwa ni mtu wa kupenda kutembea sehemu mbalimbali, lakini sasa hivi hawezi kwenda popote akiwa mwenyewe.

Jama alitangaza mbele ya mahakama kuwa amemsamehe aliyempiga na kusema kuwa utofauti wa rangi au lugha au dini uliopo miongoni mwa binadamu si kitu kwani wote ni wamoja na wanapigania haki moja.

Aidha, wakati akitangaza msamaha huo alimwambia Jodie Burchard-Risch anaamini kuwa atachagua kuwa na upendo kwa kila mmoja badala ya kuwa na chuki ambayo mwisho wa siku haimsaidii jambo lolote bali ni kuleta madhara.

Dini yangu inanifundisha kusamehe ili na mimi nisamehewe, nisipokusamehe ni mimi sitasamehewa, haijalishi nimejifunga nini kichwani, rangi yangu ni ipi au lugha gani nazungumza lakini sote ni binadamu, alisema Jama.

Jodie Burchard-Risch amehukumiwa kwenda jela miezi 6 na atakuwa chini ya uangalizi kwa maika mitano.

Hapa chini ni video ya Jama alipokuwa akitangaza kumsamehe aliyempiga na bilauri usoni mbele ya Mahakama Minnesota, Marekani.