DAVID KAFULILA AIKACHA NCCR-MAGEUZI NA KUTIMKIA CHADEMA

Leo Decemba16,2016 nimemwandikia barua Katibu Mkuu wa NCCR-MAGEUZI, kiustarabu kumjulisha mambo manne;



1.Nakishukuru chama na viongozi kwa muda wote tuliokuwa pamoja katika kujenga chama.

2.Nimeamua kujivua uanachama na hivyo Uongozi wa Katibu Mwenezi Taifa

3.Pamoja na ukandamizwaji haki kwenye vyombo vya utoaji haki bado siwezi kukata tamaa kuishi ndoto yangu ya kupigania mabadiliko ninayoamini kwa taifa langu

4.Mabadiliko hayo yanaweza kutekelezwa kwa wepesi kwa kwa wenye dhamira kuunganisha nguvu katika chama kimoja cha upinzanI ambacho kinajipambanua kwa mipango na mikakati ya kuleta mabadiliko hayo, ambacho kwa maoni yangu ni CHADEMA. Hivyo natangulia huko.

David Z, Kafulila