George Lwandamina: YANGA TULIZENI MIZUKA



Dar es Salaam. Kocha wa Yanga, George Lwandamina amesena licha ya timu yake kufungwa mabao 2-0 na JKU ya Zanzibar juzi, ameona mwanga kwenye kikosi chake.Lwandamina aliwatoa hofu mashabiki akieleza kuwa vijana wake watakuwa tishio kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara unaoanza Desemba 17.

Kocha wa Yanga, George Lwandamina


Aliwataka mashabiki watulize akili kwani mambo mazuri yanakuja, watatisha kwenye ligi hiyo na hata za kimataifa.

Lwandamuna aliyetua Yanga hivi karibuni akichukua mikoba ya Hans Pluijm alisema lengo la mchezo wa juzi lilikuwa kuwaangalia wachezaji wake na kujua wapi kuna kasoro na upungufu kabla ya mzunguko wa pili.

Alisema ndiyo maana alitumia vikosi viwili tofauti kwenye mchezo huo kwani hana kikosi cha kwanza hadi sasa. Kipindi cha kwanza, kocha huyo aliwaanzisha wachezaji wengi waliokuwa wakikaa benchi chini ya Pluijm na kikosi hicho kufungwa mabao 2-0 na baadaye aliingiza nyota wa kikosi.

Kabla ya kuanza kipindi cha pili aliwaingiza, Deogratius Munishi Dida, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Vincent Bossou, Andrew Vincent, Justine Zulu, Deus Kaseke, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Simon Msuva walianza kwa kupasha misuli na kuamsha shangwe za mashabiki, waliosema hiyo ndiyo Yanga.

Hata hivyo, kikosi hicho hakikuchomoa mabao ya JKU na kuwafanya mashabiki kuondoka uwanjani wanyonge.

Kiungo Zulu aliyepachikwa jina la ‘mkata umeme’, alionyesha kiwango kizuri cha kutoa pasi, kukaba jambo lililofanya mashabiki kumshangilia. “Mashabiki hawapaswi kuwa na wasiwasi lengo la mchezo huu ni kuwaona wachezaji na kujua upungufu kwenye kikosi changu kabla ya kuanza mzunguko wa pili wa ligi.