Humphrey Polepole kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM



Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM(NEC) imemteua Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Humphrey Polepole kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi. Ndugu Humphrey Polepole alikuwa mmoja ya Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Uongozi wa Jaji Joseph Sinde Warioba.



Baadae aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma na baadae akateuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya mpya ya Ubgungo.

Nafasi hiyo ilikuwa wazi tangu Nape Moses Nnauye ateuliwe na Rais Magufuli kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo.