Mwanzilishi wa Mtandao wa JamiiForums, akamatwa na Polisi kwa kukataa kutoa taarifa za siri za watumiaji wa mtandao huo



Anyimwa dhamana atakaa rumande mpaka kesho atakapofikishwa mahakamani. Maxence ameendelea kushikilia msimamo kuwa ni uvunjwaji wa Sheria na Haki za wananchi kufanya hivyo.



Maxence Melo anakamatwa huku kukiwa na Kesi ya Kikatiba dhidi ya taarifa ambazo Jeshi la Polisi wanazitaka, kesi namba 9 ya mwaka 2016 dhidi ya Jamii Media dhidi ya polisi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kesi ambayo mahakama kuu itatolea hukumu, tarehe 20 Februari.