Askofu mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Josephat Gwajima na wenzake watatu wataendelea kujitetea leo katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es salaam
Wakili wa serikali, Joseph Maungo alimweleza,Hakimu mkazi mkuu, Goefrey Mwambapa kuwa kesi ilipangwa jana kwa ajili ya utetezi na wapo tayari
Gwajima pamoja na wenzie wanatetewa na Wakili Peter Kibatala na Faraja Mangula, ambao wote walikuwepo mahakamani jana lakini hakimu mfawidhi, Cyprian Mkehe anayeisikiliza kesi hiyo hakuwepo
Katika kesi hiyo Askofu Gwajima anakabiliwa na shtaka la kushindwa kuhifadhi silaha na risasi anazomiliki kihalali katika usalama
Aidha Wenzie George Milulu, George Mzava (Msaidizi wake) na Yeriko Bihagaze wanakabiliwa na mshtaka ya kumiliki bastola aina ya Berretta na risasi 20 kinyume na sheria