MANJI: NATAKA KUISUKA UPYA YANGA SC


Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji amesema kuwa anataka kusuka upya timu hiyo ili wawezekufanya vizuri kwenye mashindao ya kimataifa

Manji ametoa kauli hiyo baada ya Yanga kukubali kipigo cha goli 4-0 kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Timu ya MC Algels ya nchini Algeria

"Niliongea na timu kabla ya kwenda Algeria lakini pia niwaambie mashabiki wetu hawapaswi kukata tamaa ni kweli tumetolewa lakini tuendelee kuipa sapoti timu yetu ili iweze kupata nafasi nyingine ya michuano ya kimataifa nataka kuisuka upya Yanga ili iwe na uwezo wa kucheza mashindano makubwa Afrika na kufika mbali," amesema Manji

Aidha Manji aliongeza kuwa kuyumba kwa timu hiyo kumetokana na matatizo aliyopata lakini anamini kuwa Yanga itarudisha makali yake licha kuwa matatizo bado hayajaisha

"Yanga ni timu kubwa Afrika na kama Mwenyekiti sitokubali kuona wanahadhirika kwa kushuka chini kimafanikio ndiyo maana nataka kurudisha ubora wa timu ili kufikia kile tulichokikusudia msimu huu" aliongeza