HAKIELIMU YATAKA WAZIRI WA ELIMU APUNGUZIWE MADARAKA

Shirika la HakiElimu limeitaka Serikali kufuta utaratibu wa sasa unaompa madaraka waziri wa elimu kubadilisha mifumo ya elimu badala yake kiundwe chombo maalum kitakachofanya kazi hiyo.



Hatua hiyo imekuja baada ya Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako kufanya mabadiliko katika astashahada na stashahada za ualimu kusimamiwa na  Necta badala ya Nacte.

Akizungumza jana (Jumatatu), Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, John Kalage amesema  licha ya shirika kuunga mkono mabadiliko yaliyofanywa na waziri lakini uamuzi huo haupaswi kufanywa na mtu mmoja.

Amesema kinahitajika chombo maalum kusimamia mifumo ya elimu kama ilivyo kwa Bodi ya Uhasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) inavyosimamia taaluma ya uhasibu.

#Mwananchi