EFM wamkwapua Twalib Omar wa Clouds TV

Vita vya EFM NA Clouds Media vinazidi kushika kasi. Baada ya Clouds FM kumrudisha mtangazaji wake wa zamani, Paul James aka PJ wiki kadhaa zilizopita, EFM wamejibu mapigo kwa kumchukua mtangazaji wa Sports Bar ya Clouds TV, Twalib Omar. Watangazaji wa EFM, Maulid Kitenge, Tunu Hassan na Maestro wakimkaribisha mtangazaji wa Clouds TV, Twalib Omar.



Twalib hajamaliza hata miezi minne kama sio mitatu Clouds TV alikoenda baada ya kuondoka Azam TV.
Usajili huo mpya umetangazwa na Maulid Kitenge ambaye kupitia ujumbe wake wa Instagram, inaonesha amempiga kijembe hasimu wake, Shaffi Dauda ambaye ni meneja wa vipindi wa Clouds FM. “Wakati unahangaika kurudisha wale wa zamani siye tunakuchukulia wengine,” ameandika Kitenge. “Karibu jembe Twalib Omar E FM na hii jezi utaitumia katika E FM jogging club yetu. #huumchezohauitajihasira msalimieni rafiki yangu Mino Raiola mwambieni kuna Jorge Mendez yeye harudishi wa zamani anachukua wapya,” ameongeza.

Hadi sasa watangazaji wengine wa Clouds FM waliopo EFM ni pamoja na Dina Marious, Gerald Hando na Ibrahim ‘Maestro’ Masoud. Pamoja na kuwarudisha watangazaji wake wa zamani Gardiner G Habash na PJ, Clouds ilimkwapua mtangazaji wa Singeli, Kicheko kutoka EFM.

Chanzo: BONGO5

Related Posts