Naibu waziri wa Afya kayaongea haya kuhusu Wazee kupata huduma ya afya bure ?



Naibu waziri wa Afya kayaongea haya kuhusu Wazee kupata huduma ya afya bure "Ni haki ya msingi kwa wazee kupata huduma ya afya bure sababu wao ndiyo walioijenga nchi hii kipindi kile walipokuwa wakulima na sasa wamezeeka na hawana pensheni. Tamko lipo linasema wazee watibiwe bure lakini utekelezaji haukuwepo na kwa serikali ya sasa tunafanya utekelezaji na huduma hii inaanza kwa wazee kuanzia umri wa miaka 60 na kuendelea na ndiyo maana tunatengeneza mfumo wa kadi za wazee ili iwe rahisi kwao pindi wanapohitaji huduma ya kiafya kwasababu ya kadi watakazo kuwa nazo"
Dk Kigwangalla Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia Wazee na Watoto akizungumza katika #Clouds360 ya #CloudsTv